MASERU: Bunge jipya lapigiwa kura nchini Lesotho
17 Februari 2007Matangazo
Wapiga kura katika Ufalme wa Lesotho hii leo wanachagua bunge jipya.Katika nchi hiyo ndogo yenye watu milioni 1.8 kiasi ya watu 920,000 wana haki ya kupiga kura.Inasemekana kuwa chama cha upinzani cha “All Basotho Congress“ kikiongozwa na waziri wa nje wa zamani,Tom Thabane kina nafasi nzuri ya kushinda.Yeye binafsi alipokwenda kupiga kura yake alisema,wananchi wa Lesotho wanataka badiliko.Lesotho inayozungukwa na Afrika ya Kusini,ilipata uhuru wake mwaka 1966 kutoka Uingereza na ni miongoni mwa nchi zilizo masikini kabisa barani Afrika.Vile vile inapambana na tatizo kubwa la UKIMWI.