Hali si shwari kwa makumi ya maelfu ya wakimbizi na wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutokana na kuendelea kufurushwa makwao kutokana na ghasia zinazochochewa na vikundi vilivyojihami mashariki mwa nchi hiyo. Mahitaji ya kibinadamu yanaongezeka kila uchao huku ufadhili kwa mashirika ya misaada ukipungua. #Kurunzi