1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schulz katika mahojiano na DW

19 Septemba 2017

Katika mahojiano maalumu na DW, mgombea wa SPD Martin Schulz, amekosoa uongozi wa Kansela Angela Merkel, na kuapa kutompigia magoti rais Tayyip Erdogan wa Uturuki, akisema hawezi kutishiwa juu ya srea ya wakimbizi.

https://p.dw.com/p/2kBb7
Deutschland wählt DW Interview mit Martin Schulz
Picha: DW/R. Oberhammer

Siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa bunge, kiongozi wa chama Social Democratic cha Ujerumani SPD, na mgombea wa ukansela Martin Schulz amemkosoa vikali rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Akiwa katika kampeni zake katika mji wa kusini mwa Ujerumani wa Freiburg, Schulz alikutana na mhariri mkuu wa DW Ines Pohl na mtangazaji Jaafar Abdul Karim.

Alisema hali ya haki za binadamu nchini Uturuki ni mbaya, na kuogeza kuwa haileti maana kwa sasa kuzungumza na Rais Erdogan, akipendekeza kufutiliwa mbali mazungumzo ya taifa hilo kujiunga na Umoja wa Ulaya.

"Nimekwishasema na narudia, kwamba kwa namna serikali ya Uturuki inavyofanya, hiwezi kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, na ikilaazimika nitaufutilia mbali mkataba wa wakimbizi kati ya umoja wa Ulaya na Uturuki na tutawahudumia wakimbizi. Lakini binfasi siko tayari kumpigia magoti Erdogan, hatuwezi kukubali kutishiwa," alisema Schulz.

Deutschland wählt DW Interview mit Martin Schulz
Mwenyekiti wa SPD na mgombea ukansela Martin Schulz akizungumza na mhariri mkuu wa DW Ines Pohl na mtangazaji Jaafar Abdul Karim, Septemba 16,2017.Picha: DW/R. Oberhammer

Apigia chapuo sheria ya uhamiaji ya Ulaya

Ikiwa atachaguliwa kuwa Kansela, Schulz anataka kuanzisha majadiliano ya wazi kuhusu sera ya wakimbizi pamoja na mataifa ya Umoja wa Ulaya yanayokataa kuwapokea wakimbizi. Mgombea huyo wa chama cha SPD ametishia waziwazi kuzinyima ufadhili nchi za Umoja wa Ulaya zinazokataa kuchukuwa wakimbizi, zikiwemo Hungary na Poland.

Katika kipindi cha miaka 7 ijayo, kutakuwepo karibu euro bilioni 900 kwa ajili ya kupatiwa wanachama tofauti wa Umoja wa Ulaya. Alisema hii ndiyo sababu wakati wa mazunguzo ya kifedha wataziambia nchi kama Poland na Hungary, ambazo zinapokea malipo makubwa kutoka bajeti ya Umoja wa Ulaya, kwamba mshikamano siyo tu kuchagua kile kinachokufurahisha, bali ni kanuni.

"Ama tunaonyesha mshikamano katika masuala yote au tusahau kila kitu," alisema Schulz. Alipendekeza pia kutekelezwa kwa sheria ya uhamiaji ya Umoja wa Ulaya inayoweka viwango makhsusi kwa kila taifa, huku ikibakisha haki ya sasa ya kupatiwa hifadhi.

Alizungumzia pia umuhimu wa kushirikiana na mataifa ya Kiafrika: "Ili kuwazuwia wasafirishaji haramu wa watu tunapaswa, ikibidi, kushirikiana na mataifa kama Niger. Hilo linawezekana tu chini ya usimamizi wa mashirika ya kimataifa, kwa sababu taratibu za kikatiba zinapswa kuheshimiwa, na kuna hatari angalau ya baadhi ya mataifa kutoweza kufuata uitaratibu wa kimataifa."

Merkel anasimamia tu hali ya sasa

Zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya uchaguzi, kura nyingi za maoni zinaonyesha kuwa wazi kuwa Schulz yuko nyuma ya Merkel na chama chake cha Christian Democraticm Unioni CDU. Pamoja na hayo lakini hajakata tamaa, na anaendelea kumshambulia Merkel.

"Merkel anaendeleza hali iliopo Ujerumani kwa kufuata moto ya "nchi ambamo tunaishi vizuri na kufurahia maisha." Yuko sahihi. Tunaishi vizuri na tinafurahia maisha katika nchi hii. Lakini pia tunahitaji maisha yawe mazuri kesho, na ndiyo sababu tunahitaji kuambia watu mwelekeo gani tunauchukuwa."

DW #Germany Decides- Zitat-Tafel Schulz
Schulz amesema hayuko tayari kumpigia magoto rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kwamba hatokubali kutishiwa na suala la wakimbizi.

Viwago vya chini vya umaarufu

Alipoulizwa iwapo amevunjwa moyo na umaarufu wake unaozidi kudidimia katika chunguzi za maoni ya wapigakura, Schulz alijibu kwamba,"nafanya vizuri kusema kweli.."

Alisema kila anapofungua magazeti na kuona uchunguzi wa maoni ya raia unampendelea anajisikia furaha, na anapofungua na kukuta hali ni mbaya hajisikii vizuri.

Lakini akaongeza kuwa katika maisha yake amekumbana na mazuri na mabaya pia. "Hisia zangu zinaniambia maoni ni maoni tu, watu watazungumza Septemba 24, na hapo ndipo tutaona, alisema Schulz.

Mwandishi: Thurau Jens/Iddi Ssessanga

Mhariri. Saumu Yusuf