1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mario Götze: msaliti au mwana mpotevu?

22 Julai 2016

Mshambuliaji wa Ujerumani Mario Götze kawaida ataonekana na baadhi ya mashabiki wa Borussia Dortmund kuwa ni “Yuda”, ambao hawajafurahishwa na habari kuwa amerejea

https://p.dw.com/p/1JUME
Borussia Dortmund Bayern München 2013 am 5. Mai 2013
Picha: picture-alliance/dpa

Wengine hata hivyo wanaamini kuwa anaweza kuwa mtu wa kujaza pengo lililoachwa na Henrikh Mkhitaryan.

Baadhi ya wachambuzi wa kandanda la Bundesliga na mashabiki wa Dortmund wanaonekana kukubaliana na msemo wa jadi kuwa “Usiwahi kurudi nyuma”:

Uamuzi wa Götze kuhama Dortmund na kujiunga na mahasimu wao wakuu Bayern Munich mwaka wa 2013 haukuchukuliwa vyema katika uwana wa Signal Iduna Park, na sasa ana kibarua cha kurejea na kujega upya mahusiano yaliyovunjika.

Lakini mashabiki wengine wengi wa BVB wakiongozwa na kocha Thomas Tuchel wameelezea matumini kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 atakuwa na mchango mkubwa "Tunatumai ataleta kipaji chake. Ningependa kumwona Mario akicheka kila wakati na tena tufahamiane vyema. Nna uhakika kuwa mara tu atapoanza kucheza, ataweza kuimarika na kuwa atadhihirisha yeye ni mchezaji wa kuvutia".

Götze alishinda mataji mawili ya Bundesliga akiwa na Dortmund kabla ya kujiunga na Bayern, lakini akashindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza chini ya kocha Pep Guardiola aliyehamia Manchester City ya England.

Mario Götze Fußball zurück zum BVB
Baadhi ya mashabiki hawakufurahia uhamisho wa GötzePicha: picture-alliance/dpa/A.Gebert

Mats Hummels pia aliondoka Dortmund akiwa mchezaji wa tatu nyota kujiunga na Bayern baada ya Götze na Robert Lewandowski. Lakini baada ya Götze kurejea Dortmund na Sebastian Rode pia kuhama Bayern na kujiunga na Dortmund, mambo yameonekana kubadilika. Itabakia kuona kama hiyo itakuwa na mchango wowote kwenye kinyang'anyiro cha taji la Bundesliga au la.

Na siku moja tu baada ya tangazo la Götze kurejea BVB, klabu hiyo imetangaza kumsaini winga wa Ujerumani Andre Schürrle kutoka mahasimu wao wa Bundesliga, Wolfsburg. Schürrle mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa miaka mitano hadi mwaka wa 2021 na ataanza kufanya mazoezi na klabu hiyo mwezi Agosti.

Alianzia mpira wake Mainz, mwaka wa 2009 kabla ya kujiunga na Bayer Leverkusen 2011 kwa miaka miwili. Alijiunga na Chelsea ya England mwaka wa 2013 kabla ya kusainiwa na Wolfsburg Januari 2015.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/Reuters/AFP
Mhariri: Iddi Sessanga