Marekani yawawekea vikwazo mabilionea wanne wa Urusi
12 Agosti 2023Matangazo
Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasema mabilionea hao ni Mikhail Fridman, German Khan, Alexey Kuzmichev na Petr Aven.
Soma zaidi:Viongozi wa Kundi la Nchi saba tajiri duniani wanakusudia kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi
Kwa tangazo hilo, inamaanisha kuwa mali zote za mabilionea hao zilizoko ndani ya Marekani zimezuiliwa na raia wa Marekani na watu wote waliomo nchini humo wamepigwa marufuku kushirikiana nao kibiashara pamoja na kampuni zinazohusiana nao. Benki ya Alfa, ambayo inachukuliwa kuwa mojawapo ya benki kubwa kabisa za kibinafsi inayomilikiwa na Alfa Group, tayari imo kwenye orodha ya vikwazo.