1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yawasilisha mkakati juu ya Afghanistan

23 Machi 2009

Rais Barack Obama aashiria mwanzo wa kuondoka Afghanistan,Je vita dhidi ya Ugaidi vitachukua mwelekeo gani?

https://p.dw.com/p/HI37
Rais Barack Obama asema bora kuondoka Afghanistan kumaliza vita na wataliban.Picha: AP / DW-Fotomontage

►Marekani imewasilisha pendekezo la kupambana vikali na makundi ya Kitaliban nchini Afghanistan kwa viongozi wa jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO, siku moja tu baada ya rais Barack Obama kuashiria kwamba ananuia kuubadilisha mkakati wake Afghanistan.Obama amesema huenda akawaondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan baada ya vita vya miaka saba. Munira Muhammad na taarifa zaidi.◄

Hali tete nchini Afghanistan imekuwa donda sugu kwa utawala huu mchanga wa Obama, na Marekani haijasita kutaka kuungwa mkono na viongozi wa jumuiya ya kujihami wa NATO. Na sasa la muhimu ni kuabiliana na waasi wa kitaliban, ndio mkakati huu mjumbe maalum wa Marekani kuhusiana na maswala ya Pakistan na Afghanistan, Richard Hoolbrooke alikuja kumuelezea katibu mkuu wa NATO Jaap De Hoop Scheffer katika mkutano mjini Brussels. mkutano huo pia ulihudhuriwa na mablozi 26..

Hoolbrooke pia alikutana na maafisa wengine wakuu wa jumuiya ya Ulaya. Mkakati mpya wa marekani ni kuimarisha kikosi cha polisi cha Afghanistan kukabiliana na waasi wa kitaliban. Pamoja na hayo Hoolbrooke..anasisitiza zaidi Washington ina imani iwapo Pakistan itashirikishwa kabisa, watakuwa wamepiga hatua kubwa Afghanistan.

'' unaweza kuwa na serikali nzuri kabisa duniani hapa KABUL....lakini iwapo hali itakuwa kama ilivyo katika katika mipaka Pakistan, basi hakutakuwa na mani Afghanistan, kwani huwezi tenganisha Pakistan na Afghanistan.

Kama kile kimeonekana kama ni kubadili msimamo,Barack Obama amesema miongoni mwa mkakati wake mpya nchini Afghanistan ni kuwa na mpango wa kuondoka,baada ya miaka saba, hata ingawa kwa sasa wataendelea kuongeza idadi ya wanajeshi licha ya kuimarisha mapambano dhidi ya waasi wa Taliban.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CBS Rais Obama alisema " wanalolenga ni mpango wa muda mrefu utakaojumuisha kuondoka Afghanistan, kwani utatuzi Afghnasitan hautokuwa rahisi.

'Lazima kuwepo na mpango madhubuti, lakini ieleweke kuondoka huku hakumaanishi kuna mvutano, ila swala la Afghanistan si rahisi, na haya si matamshi yangu ni ya makamanda walio nchini humo.''

Mwezi jana Obama alitangaza Marekani itawatuma wanajeshi 17,000 zaidi Afghanistan, licha kwamba makamanda walihitaji wanajeshi wa ziada 30,000 kukabiliana na machafuko katika baadhi ya maeneo nchini humo.

Nchini Pakistan, Rais Asif Zardari ameitaka Marekani na Uingereza kuisadia Pakistan kupigana na makundi ya kigadi nchini mwake.

Mwandishi :Munira Muhammad/AFPE

Mhariri :Saumu Mwasimba