Marekani yailenga China na vikwazo kuhusu watoto wa Tibet
23 Agosti 2023Marekani imetangaza vikwazo vya kusafiri dhidi ya maafisa wa China wanaofanya kile ilichokiita kuwa ni kulazimishwa watoto wa jimbo la Tibet kuingia katika mifumo ya nchi hiyo.
Watalaamu wa Umoja wa Mataifa wanasema watoto milioni moja wametenganishwa na familia zao katika eneo hilo.
Fahamu zaidi juu ya : Tibet na China
Katika msururu wa karibuni wa hatua za Marekani dhidi ya Beijing licha ya kuanzishwa upya kwa mazungumzo ya ngazi ya juu, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amesema Marekani itafuta vibali vya kusafiria vya maafisa wa Kichina wanaohusika na sera hiyo ya shule za serikali za mabweni.
Blinken amesema sera hizo za shuruti zinakusudia kuondoa tamaduni tofauti za Tibet za lugha na kidini kati ya vizazi vichanga vya Watibet.
Soma pia: Wajumbe wa China na Dalai Lama wakutana kuhusu Tibet
Wizara ya Mambo ya Kigeni ya China imesema uamuzi huo mbaya wa Marekani unapaswa kubatilishwa mara moja.
Msemaji wa wizara hiyo Wang Wenbin ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa vinginevyo, China itatoa jibu thabiti na lenye nguvu.