SiasaMarekani
Marekani yaunga mkono mahakama dhidi ya Urusi
29 Machi 2023Matangazo
Hatua ilioongeza kasi ya kushtaki uhalifu huo kwa mara ya kwanza baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Kwa upande wa Umoja wa Ulaya nayo imeunga mkono mahakama maalumu ambayo inaweza kumfungulia mashitaka mapya Rais Vladimir Putin na itakuwa ni msako wa kisheria baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC kutoa hati ya kukamatwa kwake kutokana na tuhuma za uhalifu wa kivita. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Marekani ambayo uhusiano wake na ICC umejaa mashaka, kuunga mkono waziwazi mahakama maalum kuhusu Ukraine na kupitia wizara yake ya mambo ya nje imesema, itashiriki kuunda "Mahakama maalum kuhusu uhalifu wa uchokozi" dhidi ya uvamizi wa Urusi kwa jirani yake Ukraine.