SiasaZimbabwe
Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya rais wa Zimbabwe
5 Machi 2024Matangazo
Tangazo hilo limetolewa jana na wizara ya fedha ya Marekani ambayo imesema vikwazo hivyo vinaulenga mtandao wa kihalifu unaojumuisha maafisa wakuu wa serikali chini ya rais Mnangagwa ambao umekuwa ukiwahujumu watu wa Zimbabwe.
Wale waliolengwa na vikwazo hivyo watazuiwa kufanya safari zisizo rasmi nchini Marekani na mali zao zitazuiliwa.
Kupitia tangazo hilo Marekani pia imesema inaondoa vikwazo jumla vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo la kusini mwa Afrika ambavyo vimedumu kwa karibu miongo miwili.
Vikwazo hivyo viliwekwa mnamo mwaka 2003 vikulenga utawala wa zamani wa Rais Robert Mugabe kufuatia sera yake ya ardhi iliyotaifisha mashamba makubwa yaliyokuwa yakimilikiwa na walowezi wa kizungu.