Marekani yatangaza msaada mpya wa kijeshi kwa Ukraine
30 Julai 2024Matangazo
Msaada huo unajumuisha silaha na risasi ambazo vikosi vya Ukraine vinasema vinazihitaji sana kwa dharura. Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, imesema katika taarifa kuwa msaada huo unajumuisha vifaa vya thamani ya dola milioni 200 vitakavyotolewa kutoka kwa shehena za sasa za kijeshi za Marekani na vitafika uwanja wa vita haraka, pamoja na vifaa vingine vipya vilivyoagizwa ambavyo vitachukua muda mrefu zaidi kuwasili. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyamesema katika taarifa aliyoituma kwenye mtandao wa kijamii kwamba anamshukuru rais wa Marekani Joe Biden, bunge la Marekani na watu wa Marekani kwa msaada huo.