1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yataka uwazi katika udhibiti wa silaha za nyuklia

Martin,Prema/ZPR4 Mei 2010

Marekani kwa mara ya kwanza imefichua idadi kamili ya makombora yake ya nyuklia.Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi, Marekani inadhibiti silaha 5,113 za nyuklia zinazoweza kupachikwa kwenye makombora.

https://p.dw.com/p/NDnJ
U.S. Secretary of State Hillary Rodham Clinton addresses the Nuclear Nonproliferation Treaty (NPT) conference at United Nations headquarters, Monday, May 3, 2010. (AP Photo/Richard Drew)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton.Picha: AP

Msemaji wa wizara hiyo, Dave Lapan amesema Marekni kwa kufichua idadi ya silaha zake, iliyowekwa siri hadi sasa, inataka kuhimiza uwazi katika jitahada za kuzuia utapakaaji wa silaha za nyuklia duniani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton alipozungumza katika mkutano wa kuzuia utapakaaji wa silaha za nyuklia mjini New York alisema, Iran inayoendelea na mradi wake wa nyuklia inadharau kanuni za kimataifa na ametoa wito wa kuichukulia hatua kali.

Iran's President Mahmoud Ahmadinejad waves after his address to the Nuclear Nonproliferation Treaty (NPT) conference at United Nations headquarters, Monday, May 3, 2010. (AP Photo/Richard Drew)
Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad.Picha: AP

Nae Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad alipotoa hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, aliituhumu Marekani kuwa inatumia silaha zake za nyuklia kuishinikiza Iran. Wajumbe wa Marekani na nchi kadhaa za Ulaya walitoka nje ya ukumbi huo.