SiasaMarekani
Marekani: Ushirikiano na Niger ni wa manufaa kwa pande zote
19 Machi 2024Matangazo
Jeshi la Niger, ambalo lilitwaa madaraka Julai mwaka jana, lilitagaza Jumamosi jioni kwamba lilikuwa linasitisha makubaliano na Marekani mara moja, lakini wanadiplomasia wanasema kulikuwepo na ujumbe mchanganyiko usio rasmi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Vedant Patel, alisema walikuwa wanawasiliana na utawala wa mpito kupata ufafanuzi juu matamshi yao na kujadili hatua zinazofuata.
Soma pia:Marekani yatathmini mustakabali wa operesheni zake Sahel.
Niger, ambayo ni mmoja ya mataifa ya maskini zaidi duniani, ilikuwa mshirika wa karibu wa mataifa ya magharibi katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa itikadi kali katika kanda ya Sahel, ambapo Marekani ilijenga kituo kikubwa cha droni kilichogharimu dola milioni 100.