Marekani yasema Israel kuongeza kivuko kuingiza misaada Gaza
8 Novemba 2024Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani kupitia msemaji wake Matthew Miller. Afisa huyo amesema baada ya hivi karibuni Israel kukifungua kivuko cha mpakani cha Erez, serikali mjni Tel Aviv inapanga kuongeza njia nyingine ya kuingiza misaada Gaza kwenye eneo la Kissifum.
Miller amesema Washington imeendelea kuwashinikiza viongozi wa Istael na kwamba wameonesha kuchukua hatua kushughulikia wasiwasi ulioelezwa na Marekani juu ya kuzorota hali ya kutu kwenye Ukanda wa Gaza.
Taarifa hiyo imetolewa katika wakati muda wa mwisho uliowekwa na Washington wa kuboreshwa hali ya kiutu kwenye eneo hilo unakaribia wiki inayokuja.
Mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa Marekani waliipa Israel hadi Novemba 13 kuboresha hali ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza au misaada kadhaa ya kijeshi kutoka Washington itazuiwa.