1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema imewaua wanamgambo 13 wa Al-Shabaab

28 Agosti 2023

Jeshi la Marekani limesema linaamini kwamba limewaua wanamgambo 13 wa al-Shabaab kusini mwa Somalia katika kile ilichokiita shambulizi la pamoja la kujilinda kufuatia ombi la serikali ya Somalia.

https://p.dw.com/p/4Vdrd
Somalia Militants Twitter
Picha: picture alliance / AP Photo

Kamandi ya Jeshi la Marekani Barani Afrika (AFRICOM) imesema ilifanya shambulizi la anga siku ya Jumamosi (Agosti 26) dhidi yakundi la al-Shabaab karibu na mji wa Seiera ulioko umbali wa kilomita 45 kaskazini magharibi mwa Kisimayo baada ya kuombwa na serikali.

Soma zaidi: Somalia yasema imewaua wapiganaji 40 wa Al Shaabab
Marekani yalipa kisasi shambulio la kigaidi Somalia

Serikali ya Somalia na washirika wake walianzisha kampeni mwaka uliopita ya kuwafukuza wanamgambo hao wenye mahusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda, ingawa kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi makubwa.

Jeshi la Somalia na washirika wake siku ya Ijumaa walifanikiwa kuukamata mji wa El Buur, ambao ni ngome kuu ya al-Shabaab katika eneo la katikati mwa nchi hiyo, hii ikiwa ni hatua muhimu katika kampeni hiyo.