SiasaVenezuela
Marekani yamtambua Urrutia kama rais mteule wa Venezuela
20 Novemba 2024Matangazo
Hii ni mara ya kwanza kumwita hivyo, ikiwa ni karibu miezi minne tangu ufanyike uchaguzi wenye utata.
Kauli hiyo ya Marekani imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje Anthony Blinken na imezusha hasira kali kutoka kwa serikali mjini Caracas, ambayo imeitaja kuwa "ujinga na upuuzi."
Soma pia: Bunge la Ulaya lamtambua Gonzalez rais halali Venezuela
Gonzalez Urrutia ameshukuru kwa kutambuliwa na Marekani akisema kuwa hiyo ni ishara inayoheshimu mabadiliko na maamuzi ya raia. Rais aliye madarakani Nicolas Maduro alidai kushinda uchaguzi huo wa Julai 28, ambao hata hivyo uligubikwa na shutuma nyingi za udanganyifu.