1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaipeleka puta Uingereza

13 Juni 2010

Marekani imeiendesha mchakamchaka Uingereza katika michuano ya fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini, kwa kuilazimisha kutoka nayo sare ya bao 1-1

https://p.dw.com/p/Npda
Mlinda mlango wa Uingereza Robert Green akishuhudia mpira ukiingia wavuni baada ya kushindwa kuudhibiti mkononiPicha: AP

Uingereza ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya nne tu ya mchezo kupitia kwa nahodha wake Steven Gerrad, lakini uzembe wa mlinda mlango wao Robert Green kulegeza mikono iliiruhusu Marekani kusawazisha bao hilo kufuatia kombora la Clint Dempse.

England - USA WM Weltmeisterschaft Flash-Galerie
Steven Gerrard akishangilia bao la kuongozaPicha: AP

Gerrad amekiri kuwa matokeo hayo yamewaweka katika nafasi ngumu ya kusonga mbele.

Kwa upande wake kiungo mwengine wa Uingereza Frank Lampard alimtetea mlinda mlango huyo akisema kila mchezaji hufanya kosa dimbani.

Hata hivyo washabiki nchini Uingereza wanaonekana kumnyooshea kidole kocha Fabio Kapelo kwa kucheza kamari kumpanga Green, langoni, badala ya mkongwe David James.

Kulikuwa na taarifa kuwa baadhi ya wachezaji waandamizi katika timu hiyo walitaka David James aanze, kwani ana uwezo wa kuwapanga mabeki.

Katika mechi nyingine, mmoja kati ya wawakilishi wa Afrika Nigeria walifungwa bao 1-0 na Argentina, huku Korea Kusini ikiwafunga Ugiriki mabao 2-0.

Mwandishi:Aboubakary Liongo