Marekani yailaumu tena yaisifu Iran kwa mchango wake kuelekea amani nchini Iraq
24 Desemba 2007BAGHDAD:
Balozi wa Marekani nchini Iraq, kwa uangalifu ,ameipongeza Iran kwa kusaidia kudhibiti ghasia za wanamgambo wa KiShia nchini Iraq.
Akizungumza mbele ya wandishi habari mjini Baghdad, Ryan Crocker, amesema kuwa Washington inaamini kuwa Iran ndio imechochea tangazo la usitishwaji wa hujuma wa kiongozi wa kidini wa Kishia wa Iraq, Moqtada al- Sadr.Aidha balozi amesema kuwa pia Iran huenda imesaidiai kwa njia fulani kuhakikisha ushwari katika maeneo ambako inaushawishi mkubwa nchini Iraq.hata hivyo ameongeza kuwa baado utawala wa Marekani unauchukulia mchango wa Irana kama usiotegemewa na hatua zake hazieleweki.
Kipindi kilichopita Washington imeilaumu Tehran kwa kutoa vifaa na mafunzo ya kijeshi kwa wapiganaji wa Kishia nchini Iraq.
Kwa mda huohuo habari kutoka Baghdad zasema kuwa treni ambayo ilikuwa ikielekea katika mji mkuu wa Iraq kutoka sehemu za mashambani imegonga gari katika kivuko kimoja na kuwauwa watu 13 waliokuwa ndani mwa gari hilo.Polisi inasema kuwa miongoni mwa walikufa ni watoto 11.Ajali hiyo imetokea mwishoni mwa juma kaskazini mwa mji wa Hilla katika eneo linalojulikana kama Al-Sayahiyah.