Marekani yaidhinisha uuzaji wa vifaa vya kijeshi kwa Taiwan
30 Juni 2023Matangazo
Hata hivyo, uuzaji huu ni mdogo kuliko ilivyotarajiwa na hautahusisha aina kadhaa za silaha za Marekani, lakini unajiri wakati Marekani na China zikijaribu kuleta utulivu katika mahusiano yao yenye misukosuko.
China inayodai kuwa kisiwa hicho ni sehemu ya himaya yake, imelaani vikali hatua hiyo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Mao Ning amesema Marekani inapaswa kuachana na harakati zozote zinazoweza kuibua upya mvutano wa kijeshi katika eneo hilo.