SiasaMarekani
Marekani yadungua kifaa kingine katika anga yake
13 Februari 2023Matangazo
Ikulu ya Marekani White House, imesema vitu hivyo vinavyoruka vilikuwa vidogo zaidi kuliko puto la Chinalililodunguliwa wiki iliyopita. China hata hivyo ilisisitiza kuwa puto hilo lilikuwa purutangi au puto kubwa la kiraia linalotumika kwa ajili ya utafiti.
Mkuu wa kamandi ya Marekani iliyoko kaskazini mwa nchi hiyo Jenerali Glen VanHerck, amewaambia waandishi wa habari kwamba sehemu ya sababu ya kudungua vifaa hivyo, ni kuimarishwa kwa hali ya tahadhari baada ya puto la kijasusi la China kugunduliwa kwenye anga ya Marekani mwishoni mwa mwezi Januari.