UgaidiNiger
Marekani yaanza tena operesheni za kupambana na ugaidi Niger
14 Septemba 2023Matangazo
Vikosi 1,100 vya Marekani vilivyotumwa nchini humo vilisalia kwenye kambi zao tangu mapinduzi ya Julai 26, 2023.
Kamanda mkuu wa Jeshi la Anga kwa vikosi vya Ulaya na Afrika Jenerali James Hecker, amesema shughuli hizo za kupambana na ugaidi nchini Niger zimeanza tena baada ya mazungumzo kati ya Marekani na viongozi wa kijeshi waliotwaa mamlaka nchini humo.
Niger ni eneo la kimkakati kwa Marekani katika vita vyake dhidi ya vikundi vyenye itikadi kali za kiislamu, na Washington imewekeza mamilioni ya dola katika mafunzo kwa vikosi vya Niger.
Kulingana na ECOWAS, tangu kuanza kwa mwaka huu watu 4,600 wameuawa katika jumla ya mashambulizi 1,800 ya makundi ya kigaidi.