Marekani yaahidi kusaidia Burkina Faso dola milioni 55
3 Mei 2024Matangazo
Msaada huo utashughulikia mahitaji ya dharura ya chakula na lishe na mahitaji mengine. Power amesema kiasi hicho cha fedha za Marakani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa kwa Burkina Faso kitafikia karibu dola milioni 158 milioni tangu 2023.
Taarifa ya Power inasema "Kuongezeka kwa migogoro na mzozo mbaya wa kibinadamu nchini Burkina Faso kunaonekana wazi kwa jamii zilizotengwa na jicho la huruma la ulimwengu."
Burkina Faso ni mojawapo ya mataifa kadhaa katika Sahel barani Afrika, eneo linalokabiliana na uasi wenye muungano na kundi la Al Qaeda ambalo limesababisha vifo vya maelfu na idadi nyingine kubwa kuyakimbia makazi yao.