1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Urusi inaendeleza silaha za kupambana na satelaiti

Sylvia Mwehozi
16 Februari 2024

Maafisa katika Ikulu ya Marekani ya White House wamesema kuwa Urusi inaaminika kuimarisha uwezo wake wa silaha za kupambana na Satelaiti.

https://p.dw.com/p/4cSQV
Msemaji wa usalama wa taifa katika Ikulu ya Marekani John Kirby
Msemaji wa usalama wa taifa katika Ikulu ya Marekani John KirbyPicha: Ken Cedeno/UPI/newscom/picture alliance

Maafisa katika Ikulu ya Marekani ya White House wamesema kuwa Urusi inaaminika kuimarisha uwezo wake wa silaha za kupambana na Satelaiti.

Msemaji wa usalama wa taifa katika Ikulu ya Marekani John Kirby, amesema maafisa wa kijasusi wa Marekani wanazo taarifa za Urusi kuimarisha uwezo wa silaha hizo lakini kwasasa hazijaanza kutumika.

Soma: Mkuu wa NATO asema kuchelewa msaada wa Marekani kwa Ukraine kunaviumiza vikosi vya Kyiv

Kirby, ameongeza kuwa licha ya kwamba taarifa hizo zinaibua wasiwasi, lakini hakuna tishio la moja kwa moja kwa usalama wa mtu yeyote. Rais wa Marekani Joe Biden ameelekeza mfululizo wa hatua za awali katika kushugulikia taarifa hizo za kijasusi, ikiwemo mawasiliano ya moja kwa moja ya kidiplomasia na Ikulu ya Urusi Kremlin.

Lakini msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov ametupilia mbali madai hayo ya Marekani akisema ni njama za kushinikiza bunge kuidhinisha ufadhili zaidi kwa Ukraine.