1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Muungano wa kijeshi wa Marekani wadungua droni za Houthi

25 Aprili 2024

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani karibu na pwani ya Yemen umedungua droni nne zilizofyatuliwa na waasi wa Houthi siku ya Jumatano.

https://p.dw.com/p/4f9mw
Ghuba ya Aden | Mashambulizi ya Houthi
Moja ya meli iliyowahi kushambuliwa na waasi wa Houthi ikizama katika Bahari ya ShamuPicha: Khaled Ziad/AFP/Getty Images

Kamandi Kuu ya Marekani CENTCOM aidha imesema kwenye taarifa yake kupitia mtandao wa X kwamba jana mchana, kwa majira ya Yemen walilidungua kombora la masafa marefu ambalo pia lilirushwa Wahouthi kutokea maeneo wanayoyatawala nchini Yemen.

Kulingana na CENTCOM, inahisiwa kwamba kombora hilo lililenga meli ya MV Yorktown, yenye bendera ya Marekani na kuongeza kuwa hakukuwa na majeruhi wala uharibifu.

Wahuthi, ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya pwani ya Bahari ya Shamu nchini Yemen, wameanzisha mashambulizi ya makombora na droni wakizilenga meli tangu Novemba, kwa madai ya kuonyesha mshikamano na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.