Marekani na Uturuki yatangaza uadui na PKK
9 Januari 2008Matangazo
WASHINGTON
Rais George Bush wa Marekani pamoja na mwenzake wa Uturuki Abdullah Gul wamewataja waasi wa kikurdi walioko kaskazini mwa Iraq kuwa maadui zao.Akizungumza na bwana Gul katika ikulu ya Marekani kabla ya kuelekea mashariki ya Kati rais Bush ameongeza kusema Ulaya itafaidika ikiwa uturuki itajiunga na Umoja wa Ulaya kutokana na nchi hiyo kuwa mpenda amani.Ameeleza kwamba Uturuki ndio daraja kati ya Umoja wa Ulaya na ulimwengu wa kiislamu.Kwa upande mwingine rais wa Uturuki ameondoa uwezekano wa kuwepo suluhisho la kisiasa katika mzozo na waasi wa Pkk walioko kaskazini mwa Iraq.