1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani na China wakubaliana kufanya mazungumzo

6 Aprili 2024

Marekani na China zimekubaliana kufanya mazungumzo ya kina kuhusiana na uwiano ulio sawa wa ukuaji.

https://p.dw.com/p/4eUji

 Hayo ni baada ya siku mbili za mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha wa Marekani Janeth Yellen na Makamu Waziri Mkuu wa China He Lifeng mjini Guangzhou.

Mazungumzo hayo, yanaashiria hatua ya hivi karibuni ya juhudi za pamoja za kuleta utulivu wa mahusiano baina ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi ulimwenguni, tangu mkutano wa mwisho kati ya Rais Joe Biden na Rais Xi Jinping Novemba mwaka uliopita.

Soma pia: Marekani yaonya dhidi ya ruzuku ya China kwa viwanda

Yellen amesema, hatua hiyo itawezesha mijadala kuhusu kukosekana kwa usawa kwenye masuala makubwa ya kiuchumi, na kwamba ananuia kutumia fursa hiyo kutetea hali ya usawa kwa wafanyakazi na makampuni ya Marekani.

Yellen hii leo anaelekea kaskazini mwa Beijing, ambako atakuwa na ziara ya siku mbili itakayohusisha majadiliano zaidi ya ngazi ya juu na viongozi wa China.