Marekani kutuma wanajeshi zaidi Afghanistan
10 Januari 2008Matangazo
WASHINGTON
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates anafikiria kutuma wanamaji wa ziada 3,000 nchini Afghanistan.
Msemaji wa wizara ya ulinzi amesema kuongeza wanajeshi hao wa Marekani kunakusudia kuimarisha vikosi vilioko nchini Afghanistan kabla ya mashambulizi yanayotazamiwa ya kundi la Taliban ya kipindi cha majira chipukizi.Wanamaji hao wanatarajiwa kuziba pengo la uhaba wa takriban wanajeshi 7,500 walioko katika mapambano nchini Afghanistan.
Hivi sasa kuna wanajeshi 26,000 nchini Afghanistan wengi wao wakiwa chini ya Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama ISAF kinachoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi NATO.