SiasaChina
Marekani kuidhinisha mpango wa uuzaji wa silaha kwa Taiwan
2 Machi 2023Matangazo
Mpango huo utajumuisha makombora kwa ajili ya ndege zake za kivita chapa F-16, wakati kisiwa hicho kikiripoti vitendo vya ukiukaji wa mamlaka ya mipaka yake na jeshi la anga la China.
Wizara ya mambo ya nje ya China imesema leo kuwa inapinga vikali uuzaji huo mpya wa silaha na kuitaka Marekani kuachana na mauzo na mawasiliano ya kijeshi na kisiwa cha Taiwan.
Marekani imesema uuzaji huo utaisaidia Taiwan katika ulinzi wa anga yake na kuboresha usalama wa kikanda.
Mauzo ya silaha hizo yanaweza kuharibu zaidi uhusiano ambao umekuwa mbaya baina ya Washington na Beijing. Mara kadhaa China imekuwa ikitoa wito wa kusitishwa mikataba kama hiyo kwa Taiwan ambayo China inadai kuwa chini ya himaya yake.