1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Uingereza zataka mjadala wa wazi kuhusu Tigray

29 Juni 2021

Marekani, Ireland na Uingereza zimetoa wito wa kuitishwa mkutano wa wazi dharura wa Baraza la Usalama la UN kwa lengo la kujadili kile kinachoendelea katika eneo la mapigano la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray.

https://p.dw.com/p/3vixk
Äthiopien Opfer des Luftangriffs in Tigrai
Picha: Million Haileselassie/DW

Marekani, Ireland na Uingereza zimetoa wito wa kuitishwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa lengo la kujadili kile kinachoendelea katika eneo la mapigano la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray, ambapo wapiganaji waasi wanaelezwa kufanikiwa kuingia katika maeneo ya mji wa jimbo hilo, Makele.

Vyanzo vya kidiplomasia vinasema mkutano huo unaweza kufanyika Ijumaa, ingawa ni jukumu la Ufarasa, ambayo kwa mwezi ujao wa Julai itashikilia urais wa baraza hilo ndio yenye jukumu la kutaja muda na tarehe ya mkutano.

Himizo la mkutano wa wazi kuhusu mzozo wa Tigray.

Äthiopien | Straßenszene in Mekele
Wakazi wa mji wa Makele, jimboni TigrayPicha: Yasuyoshi Chiba/AFP/Getty Images

Tangu kuanza kwa vita vya Tigray Novemba mwaka uliopita, mataifa ya Magharibi hayajaweza kufanya mkutano wa wazi kuhusu jimbo hilo, ambapo mataifa mengi ya Afrika, China, Urusi na mengineyo yanautazama mgogoro huo kama kuingilia masuala ya ndani ya Ethiopia.

Jana Jumatatu, serikali ya Ethiopia ilitangaza kusitisha mapigano jimboni Tigray wakati wapiganaji waasi wakiingia katika mji mkuu wa Makele na kuzusha nderemo na vifijo vya furaha. Tangazo hilo linatolewa wakati Umoja wa Mataifa unasema  mzozo huo uliodumu kwa takriban miezi minane sasa umeisukuma idadi ya watu zaidi ya 350,000 katika kitisho cha njaa.

Mkutano wa mwisho wa ndani wa Baraza la Usalama uliketi Juni 15, kama ilivyo kwa mingine tangu mzozo huo uanze. Mgororo wa Tigray ulianza Novemba, baada ya Rais Abiy Ahmed kupeleka jeshi katika eneo hilo kwa lengo la kuuondoa uongozi wa jimbo kwa wakati huo.

Chanzo: AFP