1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani inaweza kuitegemea Ulaya

6 Novemba 2012

Ikiwa Wamarekani wanafikra sawa kama walivyo wakaazi wa barani Ulaya basi bila shaka Obama hahitaji kuwa na wasiwasi wowote katika uchaguzi huu wa rais.

https://p.dw.com/p/16dSW
Barack Obama akiwa Iowa kwenye kampeini
Barack Obama akiwa Iowa kwenye kampeiniPicha: Reuters

Utafiti wa maoni uliofanywa na shirika la Ujerumani la Marshall katika kipindi cha msimu wa kiangazi ambapo ilidhihirika asilimia 75 ya watu barani Ulaya wanamuunga mkono Barack Obama wakati mpinzani wake Mitt Romney akiungwa mkono na asilimia 8 tu ya waliohojiwa katika utafiti huo wa maoni.

Hata hivyo nchini Marekani rais Obama yuko katika hali ngumu kwasababu harakati za mpinzani wake Mitt Romney za kuingia Ikulu zinaweza kufanikiwa.Kufuatia hali hii uchaguzi huu unafuatiliwa kwa makini barani Ulaya kwasababu ikiwa uongozi utabadilika bila shaka atakayeingia madarakani atalazimika kuuzingatia uhusiano kati ya Ulaya na Marekani.

Mitt Romney akiwa kwenye kampeini New Hampshire
Mitt Romney akiwa kwenye kampeini New HampshirePicha: Reuters

Umuhimu wa Uhusiano kati ya EU na Marekani

Kwa Umoja wa Ulaya hapana shaka uhusiano wake ni muhimu na nchi hiyo juu ya sera za nje kwa jumla na hali pia ni kama hiyo upande wa Marekani,anaamini Sarah Ludford kaimu mwenyekiti wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya unaohusika na masuala ya nje katika Bunge la Ulaya.Ludford anasema suala muhimu katika pande zote mbili baada ya uchaguzi huu litakuwa ni hali ngumu ya kiuchumi inayoshuhudiwa.

Pamoja na hayo ndani ya Marekani uchaguzi huu unahusu zaidi sera za ndani ya nchi hiyo kama alivyobainisha mwenyekiti wa shirika la utafiti wa maoni la Ujerumani la Marshall tawi la mjini Brussels,Ubelgiji.Anasema kinachoonekana Marekani ni kwamba wagombea wote wawili wamejaribu kujiwekea mpaka kati yao na hali ilivyo barani Ulaya.

Hata hivyo Warepublican na Wademokrats wanafahamu fika kwamba watu wa Ulaya wamewekeza kwa kiasi kikubwa nchini Marekani na kutokana na hilo ni wazi rais atakayechaguliwa atalazimika kulipa umuhimu suala hilo na kuona mchango wa Ulaya katika ukuaji wa uchumi na soko la ajira la Marekani.

Nembo ya Umoja wa Ulaya
Nembo ya Umoja wa UlayaPicha: Getty Images

Dhima ya EU kwa Marekani

Hakuna kwa hivyo mgombea yoyote nchini Marekani atakayeweza kupuuza jukumu muhimu la uhusiano kati ya Ulaya na Marekani wakati atakapochukua hatamu za uongozi,na fauka ya hayo baadhi ya waangalizi barani Ulaya wanasubiri kwa hamu kuona ikiwa uhusiano huo utaimarika zaidi.

Sarah Ludford kaimu mwenyekiti wa ujumbe unaohusika na masuala ya nje katika bunge la Ulaya anasema Ulaya haipaswi kuachia uhusiano kati ya Marekani na Asia uendelee kuwa thabiti kuliko ilivyo kati ya Ulaya na nchi hiyo ya Marekani ingawa ni suala lisilopingika kwamba bara la Asia ni muhimu sana kwa Marekani na hasa China.Na China pia inabakia kuwa muhimu vile vile kwa bara la Ulaya.

Mwandishi: Impey,Joana/Brussels/Saumu Yusuf

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman