SiasaMarekani
Marekani imetangaza msaada wa mwisho wa silaha kwa Ukraine
28 Desemba 2023Matangazo
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema msaada huo wa mwisho wenye thamani ya dola milioni 250, unajumlisha mifumo ya ulinzi wa anga na makombora.
Rais Joe Biden amefanya kuiunga mkono Ukraine kuwa kipaumbele na silaha za Marekani na msaada wa kifedha umekuwa muhimu katika kuisaidia Ukraine inayoungwa mkono na mataifa ya Magharibi katika vita vyake dhidi ya Urusi.
Hata hivyo Warepublikan wenye msimamo mkali wameongoza juhudi za kuzuwia msaada zaidi wakiwataka Wademokrat wakubali kwanza kupitisha hatua kali za kuzuwia uhamiaji haramu kwenye mpaka wa kusini wa Marekani.