1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Droni za Iran zashambulia meli ya wafanyabiashara

Hawa Bihoga
24 Desemba 2023

Marekani imesema Iran imefanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye meli ya wafanyabiashara katika bahari ya Arabia karibu na pwani ya India jana Jumamosi.

https://p.dw.com/p/4aXa7
Usalama | Meli ya jeshi la wanamaji Marekani ikirambaa katika Bahari Nyekundu
Meli ya jeshi la wanamaji Marekani ikirambaa katika Bahari NyekunduPicha: Gunnery Sgt. Jeffrey Cordero/U.S. Marine Corps/abaca/picture alliance

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imeeleza kwamba meli hiyo ya MV Chem Pluto, iliokuwa ikipeperusha bendera ya Liberia ilikuwa imebeba mafuta na kemikali, lakini hakuna vifo vilivyoripotiwa hadi sasa ingawa moto uliosababishwa na shambulio hilo ulidhibitiwa.

Nayo wizara ya Ulinzi India ilisema meli hiyo iliyotia nanga katika pwani yake ilitokea Saudi Arabia kuelekea mji wa kusini mwa India wa Mangaluru. 

Soma pia:Marekani yazindua muungano wa ulinzi wa Bahari ya Shamu kulinda meli dhidi ya mashambulizi ya waasi wa Houthi

Tangu kuanza kwa vita katika Ukanda wa Gaza, meli katika Bahari Nyekundu zimekuwa zikishambuliwa mara kwa mara na waasi wa Kihouthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran.

Hata hivyo Iran imeionya Marekani na washirika wake kwamba safari zaidi za kimataifa zinaweza kufungwa katika ujia huo wa bahari.