Ruto na Museveni kupatanisha Ethiopia na Somalia
1 Desemba 2024Matangazo
Rais William Ruto wa Kenya na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni wamesema wako tayari kuchukuwa jukumu hilo, huku Ruto akifafanuwa kwamba,ni kwasababu usalama wa Somalia unachangia kwa nafasi kubwa uthabiti wa kanda hiyo, pamoja na mazingira ya uwekezaji na biashara. Ethiopiaambayo haina bahari na ambayo ina maelfu ya wanajeshi wake ndani ya Somalia wanaopambana dhidi ya wanamgambo wa Alshabab wanaofungamana na kundi la Alqaeda, imeikasirisha serikali mjini Mogadishu kutokana na mpango wake wa kutaka kujenga bandari katika jimbo lililojitenga na Somalia la Somaliland.