Marais wa Kongo na Rwanda wajadili suali la mashariki ya Kongo
26 Septemba 2012Matangazo
Clinton aliwasisitizia viongozi hao wawili kuutatua mgogoro kuhusiana na suala la waasi katika eneo hilo.Aidha leo marais hao wanatazamiwa kukutana na viongozi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika mkutano maalum juu ya mzozo katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.Rais Kabila aliyetoa hotuba yake hapo jana mbele ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa ameutaka Umoja huo utimize wajibu wake katika kuwashinikiza watu na nchi zinazohusika na machafuko ya Kivu.Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo yuko New York na ametutumia taarifa ifuatayo.
(Kusikiliza ripoti bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Saleh Mwanamilongo
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman