Karibu kwenye kipindi cha Vijana Mchamchaka, Miaka ya hivi karibuni utamaduni wa kutakiana kheri ya kuzaliwa umebadilika hasa baada ya kuwepo kwa ongezeko la watumiaji wa mitandao ya kijamii na majukwaa ya Kidijitali.
Vijana ambao ndio watumaiji wakubwa wa mitandao na majukwaa hayo sasa wameyageuza kuwa kama eneo la kutakiana kheri ya siku ya kuzaliwa. Baadhi huenda mbali zaidi na kupiga picha maalumu kwaajili ya siku ya kuzaliwa na kuwatumia jamaa na rafiki zao ili wazipakie mitandaoni na kuambatanisha ujumbe wa kuwatakia Kheri.
Mitandao hiyo hiyo sasa imegeuka kuwa sehemu ya kupimana urafiki, undugu na kwamba mtu asipokutakia heri ya kuzaliwa kwa kupakia picha yako kwenye mitandao ya kijamii au majukwaa ya kidijitali basi unaamini kwamba haumjali au urafiki wenu una walakini.. Vijana mchaka mchaka inawauliza kuhusu haya yanayoendelea.
Je, wewe una maoni gani juu ya hili?.