1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO : Clinton aanza ziara ya kupiga vita UKIMWI Afrika

18 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtc

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amewasili Msumbiji hapo jana akiwa katika kituo cha kwanza cha ziara yake ya mataifa sita ya Afrika na kutangaza mchango wa msaada dola milioni 50 kwa nchi hiyo katika vita dhidi ya virusi vya HIV na UKIMWI barani Afrika.

Clinton anatumai Wakfu wake utasaidia kuwapa tiba za madawa nafuu ya kurefusha maisha zaidi ya watoto 60,000 wanaoteseka na virusi vya HIV na UKIMWI katika nchi za kimaskini duniani.

Rais huyo wa zamani alisema hapo mwezi wa April Wakfu wake utatumia dola milioni 10 mwaka huu kuwapa tiba watoto 10,000 walioathirika na virusi vya HIV na UKIMWI katika nchi za kimaskini hususan kwenye maeneo ya vijijini barani Afrika.

Clinton mwenye umri wa miaka 58 aliemaliza muda wake madarakani hapo mwaka 2001 pia atatembela Lesotho,Afrika Kusini Tanzania,Kenya na Rwanda.