Maporomoko yanayovutia zaidi duniani
Maji mara nyingi huwavutia watu. Hasa wakati yakiingia kwa nguvu kwenye vilindi. Hapa kuna maporomoko kumi ya kuvutia ya maji - kuanzia yale ya Niagara hadi mapromoko ya Rhine.
Maporomoko ya Viktoria, Zambia/Zimbabwe
Maporomoko ya Victoria ni turathi ya dunia na yapo katika nchi mbili za Afrika: Zambia na Zimbabwe. Yakiwa na upana wa mita 1708 (5604 ft), yanachukuliwa kuwa maporomoko ya maji mapana zaidi ulimwenguni. Yana hadi mita za ujazo 10,000 za maji. Lakini Zambezi haina uwezo wa kuchukua maji mengi kila wakati. Katika msimu wa ukame, maji hupungua sana.
Maporomoko ya Niagara, USA/Canada
Maporomoko ya Niagara yaliyoko mpaka wa Marekani na Canada yalipewa jina la India la "maji yanayounguruma": kulingana na msimu, mita za ujazo za maji huwa 2,800 hadi 5,700 kwa sekunde (98,881 hadi mita za ujazo 201,293 kwa sekunde) na kumwagika kwenye vilindi hivi. Maporomoko ya Niagara yana milango mitatu ya maji: Maporomoko ya Marekani, Maporomoko ya Bridal Veil na maporomoko ya Horseshoe.
Maporomoko ya Iguazú, Brazil/Argentina
Na maporomoko mengine yanayojikua katika mataifa mawili: Yapo kati ya Brazil na Argentina. Hapa, maporomoko 275 huingia ndani ya bwawa lenye urefu wa mita 700 na upana wa mita 150. Kivutio hiki cha asili pia kimetangazwa kuwa turathi ya Dunia.
Maporomoko ya Ban Gioc Detian, China/Vietnam
Maporomoko ya Ban Gioc Detian yako kwenye mpaka kati ya China na Vietnam. Quy Xuân humwaga maji katika eneo la upana wa mita 300 wa ukuta wa mwamba wa zaidi ya mita 50. Mto huu huchukua kiwango kikubwa cha maji kati ya Mei na Septemba. Jambo la kipekee juu yake ni kwamba mazingira yake ni kama ndoto - kama mazingira ya filamu ya kufikirika.
Maporomoko ya Angel Falls, Venezuela
Ni maporomoko ya kina kirefu zaidi duniani yapo mita 979 (3,211 ft) kutoka kilele cha mlima Auyan-Tepui huko Venezuela. Yanatokana na Mto wa Río Churún. Yanapomwagika chini, maji huonekana kama matone madogo ambayo hugeuka kuwa mto unaoenda kwa kasi. Salto Ángel, kwa Kispaniola, ni sawa na Maporomoko ya Malaika. Sio rahisi kuyafikia - hufikika tu kwa ndege ama safari ya siku moja ya boti.
Maporomoko ya Gullfoss, Iceland
Iceland hutambulika kama kama kisiwa cha moto na barafu. Ni mahali ambapo kuna barafu na kuna maji mengi. Vivyo hivyo kwa mto mkubwa kabisa Gullfoss (Maporomoko ya Dhahabu). Una upana wa mita 229. Yako katika njia kunakopatikana vivutio vya maduara ya dhahabu na yanafikika kirahisi. Ni njia inayoongoza kwenye eneo ambalo watalii wanaweza kuyafurahia maporomoko ya maji kwa karibu.
Maporomoko ya Seljalandsfoss, Iceland
Iceland ina maelfu ya maporomoko ya maji. Lakini Seljalandsfoss yaliyoko kusini mwa kisiwa hicho ndio maarufu zaidi. Hapa wageni wanaweza maporomoko wakiwa nyuma ya maji, lakini pia mazingira yake. Na hususan nyakati za jioni, rangi huonekana kali sana. Hufaa sana kwa picha. Maporomoko hayo ya maji yana urefu wa mita 66 na maji yake hutokea Mto wa Seljalandsá.
Maporomoko ya Ouzoud, Morocco
Maporomoko ya Ouzoud kwenye ukingo wa Milima ya Atlas ndio milango ya maji ya juu zaidi na yenye maji mengi huko Moroko. Maporomoko ya maji madogo madogo humwagika mita 110 juu ya miamba yenye rangi nyekundu na mwishowe hutiririka ndani ya ziwa dogo. Wageni wanaweza kushuka kutoka juu kupitia njia ya miguu.
Hifadhi ya taifa ya maziwa Plitvice, Croatia
Maziwa ya Plitvice pia ni sehemu ya turathi ya Ulimwengu iliyotajwa na UNESCO na ni ukumbusho wa watalii wa Croatia. Maporomoko hayo yanaunganisha maziwa 16 yaliyopangwa kwa hatua. Hifadhi hiyo ya kitaifa iliyo na maziwa na maporomoko ya maji mengi inaweza pia kutembelewa kupitia barabara zinazokwenda mlimani, kwa boti au kwa treni ya watalii.
Maporomoko ya Rhine, Uswisi
Maporomoko ya Rhine huko Schaffhausen, kilomita chache kutoka Ziwa Constance, yana urefu wa mita 23 na upana wa mita 150. Wageni wanaweza kuona uzuri wa asili ya eneo hilo kutoka maeneo kadhaa. Sehemu nyingine ya kuvutia ni jumba kasri dogo la Wörth, ambalo liko kwenye kisiwa. Maji mengi yanaweza kuonekana kwa uzuri zaidi moja kwa moja kutoka kwenye boti.