Mapigano yazuka baina ya jeshi la Kongo na waasi wa M23
28 Machi 2022Maelfu ya wakimbizi kutoka katika baadhi ya vijiji vya kando na milima ya chanzu na runyoni wameonekana tangu asubuhi ya leo juma tatu wakivuka mpaka kuelekea nchi jirani ya uganda kufuatia mapigano makali yanayo endelea hadi muda huu kati ya jeshi la Congo na kundi la waasi wa M23 .
Vyanzo kutoka asasi zairaia vimethibitisha kutekwa upya kwa milima ya runyoni na chanzu wilayani rutshuru ambayo walikuwa wanatumia kama ngome yao kuu chini ya kamanda sultani makenga ,mwaka wa 2012 habari ambazo bado jeshi la congo kuthibitisha.
Kuzuka upya mapigano haya kati ya pande zote hizo mbili kumewatia hofu wanaharakati haki za bianadamu ambao wameitaka kamati ya kimataifa kuingilia kati mzozo huo unao weza kuyaathiri mataifa jirani kama anavyo fafanua KUSUDI mapendo wa kundi la CADH.
Soma pia→Rwanda na DRC zachunguza kurudi kwa wapiganaji wa M23
Machafuko yasiokwisha
Hadi tunapo enda hewani na matangazo haya, jeshi la congo FARDC laendelea kurusha mabomu kuelekea maeneo ya milima inayo kaliwa sasa na kundi hilo la waasi wa M23 ambao mara kadhaa wamekuwa wakiishutumu serikali ya congo kwa kuvunja mapatano kati yao ambayo ilikuwa ni njia pekee yakuleta amani upande wa mashariki.
Kurejea kwa kundi la M23 kunaripotiwa wakati serikali ya rais wa DRC Felix Tshisekedi inapambana na waasi kutoka uganda wa ADF katika wilaya ya beni na ituri operesheni ambazo hadi sasa hazija leta mafanikio makubwa.