SiasaSudan
Mapigano yazidi kupamba moto katika mji mkuu wa Sudan
5 Juni 2023Matangazo
Makubaliano hayo yalisimamiwa na Marekani na Saudi Arabia. Mapigano huko Khartoum yamesababisha uharibifu mkubwa, vitendo vya uporaji, kuathirika kwa huduma za afya, kukatika kwa umeme na maji, na kupungua kwa usambazaji wa chakula.
Soma pia: Barazala la Usalama lataka vita visitishwe Sudan
Wanaharakati nchini humo wamesema pia kuwa ghasia zilizuka katika jimbo la Darfur Kaskazini na kusababisha vifo vya watu 40.
Mzozo huu wa madaraka kati ya majenerali wawili hasimu ulioanza Aprili 15 mwaka huu umesababisha mgogoro mkubwa wa kibinaadamu ambapo zaidi ya watu milioni 1.2 wamekuwa wakimbizi wa ndani huku wengine 400,000 wakikimbilia nchi jirani.