1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mapigano yaongezeka mashariki mwa Ukraine

16 Julai 2023

Ukraine imesema, mapigano yameongezeka katika upande wake wa mashariki wakati vikosi vyake na Urusi vikipambana katika angalau maeneo matatu.

https://p.dw.com/p/4TyDF
Ukraine, Saporischschja | Soldatinnen trainieren für den Einsatz an der Front
Picha: Ercin Erturk/AA/picture alliance

Kyiv ilifanya shambulio lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu ili kuchukua tena udhibiti katika eneo lililokaliwa na Urusi mwezi uliopita na limesonga mbele katika sehemu za mashariki na kusini.

Soma pia: Putin: Urusi ina hifadhi ya kutosha ya mabomu ya mtawanyiko kujibu mashambulizi

Kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram Naibu Waziri wa Ulinzi Hanna Maliar amesema kwamba vikosi vya Urusi vimekuwa vikishambulia kuelekea Kupyansk katika mkoa wa Kharkiv kwa siku mbili mfululizo.

Maliar amesema majeshi ya Urusi na Ukraine yalikuwa yakipigana karibu na jiji lililoharibiwa la Bakhmut lakini vikosi vya Ukraine vilikuwa vikisonga mbele taratibu katika upande wake wa kusini.