Mapigano yaendelea Yemen
10 Julai 2015Mapigano hayo yalianza saa kadhaa kabla ya kuanza kutekelezwa mpango wa kusitisha mapigano.Ndege za kivita zimeshambulia maeneo ya waasi wakishia katika mkoa wa kati al-Baida na Mareb upande wa mashariki, na kusabisha idadi isiyojulikana ya vifo,Walisema wakaazi.
Afisa mmoja wa ndani alisema waasi, wanongozwa na askari watiifu wa rais wa zamani Ali Abdullah Saleh,waliyashambulia maeneo kadhaa ya makazi katika mji wa Taiz, mji ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini Yemen.
Wakati huo huo pande kuu zinazopigana zimetakiwa kusitisha mapigano kuanzia usiku baada ya mapigano mazito juu ya ardhi na mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la muungano linaloongozwa na Saudi Arabia bila ya kuchoka .
Mpango wa kusititisha mapigano unakuja wakati ambapo Waislam wapo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na una malengo ya kuwapatia misaada raia ya Yemen mlioni 21. Pande zote walisema wanamatumaini kusitisha mapigano kamili ungefuata.
Kwa mujibu wa afisa mmoja , wapiganaji wa Houthi uliyashambilia maeneo ya makazi katika bandari ya kusini ya Aden usiku kucha na kusonga mbele zaidi Yemen mashariki jangwani katika mji wa Hadramawt, kwenye kituo cha rasilimali ya nchi hiyo cha mafuta, yenye mapigano wanamgambo wa kikabila.
Kampeni inayoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya wapiganaji hao wa Kishia, iliyalenga maeneo yao katika mji mkuu sanaa leo , baada ya kuishambulia miji ya kati na kusini jana usiku .
Muungano huo wa mataifa ya kiarabu umewashambulia wapiganaji wa Houthi na wanajeshi washirika walio watiifu kwa rais wa zamani Ali abdullah saleh, tokea Machi 26, kam a sehemu ya juhudi za kumrejesha madarakani Rais Hadi aliyekimbilia uhamishoni Saudi Arabia. tangu wakati huo ,mashambulizi ya kutokea angani na mapigano ya nchi kavu kati ya pande zinazohasimiana ndani ya Yemen yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000.
Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa watu milioni 21 wanahitaji kusaidiwa nchini Yemen-idadi hiyo ni sawa na asilimia 80 ya wakaazi jumla wa nchi hiyo.
Mwandishi: Salma Mkalibala, dpae, rtr
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman