Mapigano yaendelea Sudan
5 Mei 2023Matangazo
Mamia ya watu wameuawa katika mapigano yaliyodumu kwa takribani wiki tatu kati ya majenerali wawili wanaohasimiana.
Mapambano yameendelea siku moja baada ya Rais wa Marekani, Joe Biden, kutishia kuwawekea vikwazo wale wanaohusika katika kudhoofisha amani, usalama na utulivu wa Sudan.
Wakati huo huo, Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), limezitolea wito serikali mbalimbali kuwaruhusu raia wanaokimbia vita Sudan kuingia kwenye ardhi zao na kutowarudisha kwenye nchi hiyo.
Soma zaidi: Marekani yatishia vikwazo vipya nchini Sudan
Elizabeth Tan, Mkurugenzi wa Ulinzi wa Kimataifa wa UNHCR, amesema wanazishauri serikali kuwatowarejesha watu Sudan kwa sababu ya mzozo unaoendelea huko.