Mapigano yaendelea Rafah huku Biden akiilaumu Hamas
14 Juni 2024Matangazo
Hali ya wasiwasi pia inaendelea kuongezeka katika mpaka wa kaskazini kati ya Israel na Lebanon, huku kundi la Hezbollah ambalo ni mshirika wa Hamas likifanya mashambulizi zaidi kuyalenga maeneo ya kijeshi ya Israel. Raia mmoja wa Lebanon ameripotiwa kuuawa katika mashambulizi hayo.
Rais wa Marekani Joe Biden amelilaumu kundi la Hamas kwa kuchelewesha kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa wiki sita, kuwachiwa mateka na ujenzi mpya wa Gaza.
Blinken ataka suluhisho la kidiplomasia kati ya Israel na Lebanon
Hata hivyo afisa mkuu wa Hamas Osama Hamdan, amesema kundi hilo linataka usitishwaji wa kudumu wa mapigano na kuondolewa kabisa wanajeshi wa Israel kutoka Gaza lakini Israel inayapinga masharti hayo ya Hamas.