1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Mapigano ya Sudan yatimiza miezi miwili tangu kuzuka

15 Juni 2023

Ndege za kijeshi zilishambulia kwa mabomu mji wa El Obeid nchini Sudan , wakati nchi hiyo leo hii ikitimiza miezi miwili tangu mzozo wa kimadaraka kati ya majenerali hasimu kuiingiza nchi hiyo katika mzozo mkubwa.

https://p.dw.com/p/4SacK
Sudan | mapigano Khartoum
Raia akikagua nyumba yake iliyoharibiwa na mashambulizi kusini mwa KhartoumPicha: AFP

Ndege za kijeshi zilishambulia kwa mabomu mji wa El Obeid nchini Sudan , wakati nchi hiyo leo hii ikitimiza  miezi miwili tangu mzozo wa kimadaraka kati ya majenerali hasimukuiingiza nchi hiyo katika mzozo mkubwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda jana Jumatano, jeshi la Sudan lilifanya mashambulizi ya anga kwa mara ya kwanza huko El Obeid mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kaskazini, kilomita zipatazo 350 kusini mwa mji mkuu, ambao umezingirwa na wapiganaji wa RSF tangu kuanza vita.

Tangu Aprili 15, jeshi la Sudan linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na Vikosi vya Msaada wa Dharura vya kijeshi vinavyoongozwa na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo vilianza makabliano kwenye mapigano ya mijini ambayo yameacha vitongoji vyote vya mji mkuu Khartoum kuharibika.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhima ya uhamiaji IOM zaidi ya watu milioni 2.2 wameyakimbia makazi yao, wakiwemo zaidi ya milioni moja kwa Khartoum pekee.