1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano mji mkuu wa Somalia

20 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dl3g

Mogadishu:

Mapigano makali kati ya wanaharakati wa Kiislamu nchini Somalia na wanajeshi wa Ethiopia, katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, yamewauwa karibu watu 20. walioshuhudia walisema wanajeshi watano wa Ethiopia, watatu wa serikali ya mpito na raia kadhaa ni miongoni mwa waliouwawa. Somalia imeingia katika mtafaruku na mapigano tangu Ethiopia ilipotuma wanajeshi mwaka 2006 kuisaidia serikali ya Somalia dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu. Waasi hao waliangushwa katika mji mkuu mwaka mmoja uliopita, lakini kungali na waliobakia , ambao wanaendesha vita vya chini kwa chini dhidi ya serikali ya mpito na wanajeshi wanaoisaidia ,kutoka Ethiopia na umoja wa Afrika.