1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSomalia

Mapigano makali yazuka Puntland Somalia

Josephat Charo
20 Juni 2023

Mapigano makali yamezuka mapema JUmanne asubuhi mjini Garowe, mji mkuu wa eneo lenye utawala wake wa ndani la Puntland nchini Somalia.

https://p.dw.com/p/4SoVz
Somalia Unruhen
Picha: Hassan Ali ElmiAFP/ Getty Images

Mapigano makali yamezuka mapema leo asubuhi mjini Garowe, mji mkuu wa eneo lenye utawala wake wa ndani la Puntland nchini Somalia. Watu wanne walioshuhudia wamesema mapigano hayo yamezuka wakati bunge lilipoanza kujadili mageuzi ya mfumo wa uchaguzi. Serikali ya Puntland imesema katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook wkamba bunge lilikuwa limepiga kura kuunga mkono mageuzi ya katiba na mijadala zaidi na kwamba kura zitafanyika. Mzee wa mji wa Garowe Farah Osman amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema mji huo umejaa wapiganaji wanaopambana na kwamba biashara na barabara zote zimefungwa.