Mapigano makali yasababisha vifo 17 Somalia
14 Desemba 2007Matangazo
MOGADISHU: Si chini ya watu 17 wameuawa katika mapigano yaliyozuka katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu. Katika mapigano mabaya kabisa kutokea tangu mwezi wa Oktoba,soko kuu katika mji wa Mogadishu lilishambuliwa kwa makombora na silaha zingine. Mashahidi wamesema,hapo kabla wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu walishambulia vituo vya majeshi ya Ethiopia yanayosaidia vikosi vya serikali ya mpito ya Somalia.