Mapigano makali yaendelea Ukanda wa Gaza
6 Desemba 2023Matangazo
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kwamba hali katika ardhi ya Palestina iliyozingirwa inazidi kuwa mbaya kadri muda unavyosonga mbele huku likisisitiza kuwa msaada unaowasili huko Gaza ni mdogo mno.
Soma zaidi: Israel yashambulia Khan Younis, kusini mwa Gaza
Maafisa wa jeshi la Israel walionukuliwa na mashirika ya habari ya AP na AFP wamesema makadirio yao ya idadi ya watu waliouawa Gaza ni sawa na yale yanayotolewa na Wizara ya Afya inayoongozwa na Hamas ambayo imesema kuwa hadi sasa watu 15,800 wameuawa.