1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano makali katika ngóme za mwisho za Gaddafi

12 Septemba 2011

Majeshi ya viongozi wepya nchini Libya yanakumbana na upinzani mkali katika ngome mojawapo ya mwisho ya watiifu wa Muammar Gaddafi. Hata hivyo,wanaujongelea mji wa Sirte, ambako ndio alikozaliwa Gaddafi.

https://p.dw.com/p/Rl6E
Former rebel soldiers gather at the frontline near the entrance of Bani Walid, Saturday, Sept. 10, 2011. Libyan fighters are signing up for a final assault on one of the last remaining bastions of Moammar Gadhafi. The volunteers are pouring in by the dozens, coming in pickup trucks from cities as far as Tripoli and Tobruk, as a deadline expired on Saturday for the pro-Gadhafi loyalists holed up inside the town of Bani Walid to surrender. (Foto:Alexandre Meneghini/AP/dapd)
Vikosi vya NTC nje ya Bani WalidPicha: dapd

Wanajeshi ya Baraza la Kitaifa la Mpito, NTC waliyompindua Gaddafi mwezi uliopita, wanasema, wanapambana vikali na kiasi ya wapiganaji 1,000 walio watiifu kwa Gaddafi katika ngome ya Bani Walid. Wakaazi wanaoukimbia mji huo, wameripoti mapigano makali barabarani huku ndege za jumuiya ya kujihami NATO zikiruka katika anga hiyo. Msemaji wa NTC, Jalil la-Galal amesema, hakuna anaejua watachukua muda gani kuuteka mji wa Bani Walid.

Libyan Transitional National Council chairman Mustafa Abdel Jalil, center, flanked with body guards tries to find his way upon his arrival at Metiga airport in Tripoli, Libya, Saturday, Sept. 10, 2011. (Foto:Francois Mori/AP/dapd)
Mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Mpito, Mustafa Abdel Jalil(katikati)Picha: dapd

Baraza hilo la mpito limesema, halitotangaza ukombozi wa Libya mpaka litakapodhibiti miji yote iliyo katika mikono ya wafuasi wa Gaddafi. Miji hiyo na wapiganaji wake walipewa hadi siku ya Jumamosi kusalim amri, lakini katika mji wa Bani Walid, wanapigana tangu siku ya Ijumaa. Vikosi vya NTC vinasema, vinakumbana na upinzani mkali kuliko vile ilivyotarajiwa, lakini vinaweza kusonga mbele kuelekea Sirte na vipo kiasi ya kilomita 90, mashariki ya mji huo ulio katika barabara kuu ya pwani inayotoka upande wa mashariki kwenda magharibi. Serikali ya mpito imepeleka vikosi zaidi Bani Walid.

Wakati huohuo, familia zilizonasa kwa majuma kadhaandani ya mji huo, zimefanikiwa kuukimbia mji huo leo hii, baada ya vikosi vya Gaddafi kuvihama baadhi ya vituo vya ukaguzi nje ya mji wa Bani Walid. Msemaji wa kijeshi wa baraza la mpito, Ahmed Bani amewaambia waandishi wa habari, wapiganaji wa Gaddafi wanawatumia raia kama ngao na wameweka makombora kwenye paa za nyumba zenye familia. Kwa hivyo, ni vigumu kwa majeshi ya NTC au NATO kushambulia.

Al-Saadi Gaddafi, Fußball-Profi und einer der Söhne des libyschen Revolutionsführers Gaddafi, trägt am 29.06.2003 eine Sonnenbrille vor dem Logo des Fußballvereins AC Perugia im italienischen Torre Alfina . Der Sohn des libyschen Diktators spielte insgesamt 28 Spielminuten in der ersten italienischen Liga. Foto: Filippo Monteforte (zu dpa Im Fokus "Al-Saadi Gaddafi: Möchtegern-Profi in Italien" vom 25.08.2011) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Saadi al-Gaddafi ameingia nchi jirani NigerPicha: dpa

Na katika nchi jirani Niger, Waziri wa Sheria Marou Adamou amesema, mtoto wa Gaddafi, Saadi, amezuiliwa baada ya kukutikana katika msafara uliovuka mpaka na uliokuwa ukielekea mji wa jangwani Agadez. Alipoulizwa kuhusu hatima ya Saadi, waziri huyo alisema, Niger itatimiza wajibu wake wa kiutu. Majirani wa Libya wanashinikizwa na nchi za magharibi, kutotoa hifadhi kwa Gaddafi wala maafisa wake wanaotakiwa kwa tuhuma za uhalifu.

Watoto wengine wawili wa kiume, Mohammed na Hannibal na binti yake pekee Aisha, wamepata hifadhi nchini Algeria. Mutassim na Khamis waliyoviongoza vikosi vya kijeshi vya tabaka la juu na Saif al-Islam alietazamiwa kumrithi baba yake wapo mbioni. Saif al-Arab ameripotiwa kuuawa wakati wa vita hivyo. Saif al-Islam na Muammar Gaddafi wanatakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague, Uholanzi kwa uhalifu wa kivita.

Mwandishi: Martin,Prema/rtre

Mhariri: Abdul-Rahman