1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mapigano makali bado yaendelea Sudan

2 Mei 2023

Mapigano makali yameendelea leo Jumanne kati ya vikosi tiifu kwa majenerali wawili mahasimu nchini Sudan licha ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4QnBj
Sudan Proteste und Kämpfe in Khartoum
Picha: AFP

Mapigano hayo yanashuhudiwa wakati zikitolewa tahadhari juu ya uwezekano wa kutokea kile kinachoitwa janga la mgogoro wa kibinadamu nchini humo huku wakishuhudiwa mamia kwa maelfu ya wakimbizi.

Jana Jumatatu afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya msaada nchini Sudan, Abdou Dieng alionya kwamba hali inageuka kuwa janga kamili.

Rais wa Kenya William Ruto aliyekuwa na mkutano kwa njia ya mtandao na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa amesema kuna haja ya kupatikana njia ya kutolewa msaada wa kibinadamu nchini Sudan iwe kuna usitishaji mapigano au la.

Kiongozi huyo wa Kenya amesema mgogoro wa Sudan umefikia katika kile alichokiita ''viwango vya Janga.''

Mamia ya watu wameuwawa na maelfu ya wengine wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi ya anga na makombora yanayorushwa na kila upande katika mji mkuu Khartoum.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW