1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapatano yafikiwa kwenye mazungumzo juu ya Korea ya Kaskazini

13 Februari 2007

Wajumbe wa nchi sita kwenye mkutano wao wa mjini Beijing wamefikia mapatano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea ya kaskazini. Chini ya mapatano hayo Korea ya Kaskazini itaanza kupunguza shughuli za uundaji wa silaha za nyuklia na badala yake itapatiwa msaada wa nishati.

https://p.dw.com/p/CHKJ
Mazungumzo juu ya Korea ya Kaskazini kuacha mpango wake wa nyuklia
Mazungumzo juu ya Korea ya Kaskazini kuacha mpango wake wa nyukliaPicha: AP

Mjumbe wa Marekani kwenye mkutano huo naibu waziri wa mambo ya nje bwana Christopher Hill amesema kuwa mapatano yamefikiwa baada ya mazungumzo ya undani na kwamba hatua sasa zinatarajiwa kuchukuliwa.

Chini ya mapatano hayo Korea ya Kaskazini itaanza kupunguza shughuli za uundaji wa silaha za nyuklia na badala yake itapatiwa msaada wa nishati.

Mjumbe wa China Wu Dawei ameeleza Korea ya Kaskazini itafunga mtambo wake wa nyuklia ikiwa pamoja ule wa Yongbyon.

Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa watarejea tena nchini Korea ya Kaskazini kufuatilia hatua za kukifunga kituo hicho wakati Korea itapatiwa tani alfu 50 za mafuta katika kipindi cha siku 60 zijazo.

Chini ya makubaliano hayo, pia Marekani na Korea ya Kaskazini zitaanza mazungumzo ya ana kwa ana ili kutatua masuala yanayozihusu nchi mbili hizo ikiwa pamoja na kuchukua hatua za kuanzisha mahusiano ya kibalozi.

Marekani pia itatafakari kuiondoa Korea katika orodha ya nchi za kigaidi.

Japan na Korea ya Kaskizini pia zitaanza mazungumzo ya ana kwa ana ili kutatua masuala yanayozihusu.

Nchi sita zilizoshiriki kwenye mazungmzo hayo zimekubaliana kuunda majopo yatakayofuatilia makubaliano yaliyofikiwa na yataanza kazi katika muda mwezi mmoja ujao na kutayarisha mazungumzo mengine tarehe 19 mwezi ujao.

Majopo hayo yatafuatilia hatua za Korea ya kaskazini za kuacha mpango wake wa nyuklia.

Kwenye mazungumzo ya mwezi septemba mwaka jana Korea ya Kaskazini ilikubali kimsigni kuacha mpango wake wa nyuklia ili kuweza kuhakikishiwa usalama na kupatiwa msaada wa kiuchumi.

Hatahivyo mapatano hayo yanapaswa kuidhinishwa na nchi sita zinazohusika na suala la Korea ya Kaskazini ikiwa pamoja na Marekani, China, Japan,Urusi na Korea zote mbili.

Mjumbe wa Marekani bwana Christopher Hilll amesema kuwa nchi yake inaunga mkono mapatano yaliyofikiwa kwenye mkutano huo. Wa Beijing

Hatahivyo bwana Christpoher Hill ameeleza kuwa mapatano hayo ni hatua ya kwanza katika kutelekeza mchakato wa kupunguza silaha za nyuklia. Amesema kuwa mapatano hayo ni hatua inayoelekea katika kuondoa silaha za nykulia lakini mambo bado hayajakamilika.

Bwana Hill amesema Korea ya Kaskazini, nchi mojawapo masikini sana duniani itapewa vivutio baada ya kufahamisha kwamba mjumbe wa nchi hiyo kwenye mazungumzo hayo Kye Gwan amekubaliana na vipengee vyote vya tamko la pamoja.

ABDU MTULLYA